John 7:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi ya watu wa Yerusalemu walisema, “Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumuua?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha baadhi ya watu waliokuwepo Yerusalemu wakasema, “Huyo ndiye mtu wanayetaka kumuua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadhi ya watu wa Yerusalemu walisema, “Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi ya watu wa Yerusalemu walisema, “Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumwua?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumuua?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi ya watu wa Yerusalemu walisema, “Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Palikuwa na wenyeji wa Yerusalemu waliosema: Si huyu, wanayemtafuta kumwua?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu watu wamoja wa Yerusalema wakasema: “Huyu si mutu yule wanayetafuta kumwua?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi baadhi ya watu wa Yerusalemi wakanena, Huyu si yeye wanaemtafuta illi kumwua?