John 7:38 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: ‘Anayeniamini mimi, mito ya maji ya uhai itatiririka kutoka moyoni mwake!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yanavyosema, vijito vya maji ya uzima vitatiririka kutoka ndani yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama mtu ataniamini, mito ya maji yenye uzima itatiririka kutoka ndani ya moyo wake. Ndivyo Maandiko yanavyosema.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: Anayeniamini mimi, mito ya maji yenye uzima itatiririka kutoka moyoni mwake!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: ‘Anayeniamini mimi, mito ya maji ya uhai itatiririka kutoka moyoni mwake!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ye yote aniaminiye mimi, kama maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: ‘Anayeniamini mimi, mito ya maji ya uhai itatiririka kutoka moyoni mwake!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye kunitegemea, kama yalivyoandikwa, mwilini mwake yeye mtatoka mito ya maji yenye uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile Maandiko Matakatifu yanavyosema: ‘Mito ya maji ya uzima yatatiririka toka ndani ya yule anayeniamini.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyonena, mito ya maji ya uzima itamtoka tumhoni.