John 8:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tena hekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawa anawafundisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alfajiri na mapema Isa akaja tena Hekaluni; watu wote wakakusanyika, naye akaketi, akaanza kuwafundisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mapema asubuhi akarudi katika eneo la Hekalu. Watu wengi wakaja kwake, naye akakaa pamoja nao na kuwafundisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tena Hekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawa anawafundisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tena hekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawa anawafundisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alfajiri na mapema Isa akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tena hekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawa anawafundisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asubuhi na mapema alipokuja tena Patakatifu, watu wote wakamwendea, naye akakaa akiwafundisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kesho yake asubui mapema akarudi tena katika hekalu. Watu wote wakamufikia, naye alipoikaa, akaanza kuwafundisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta assubuhi ilipokucha akaingia tena hekaluni, watu wote wakamwendea: nae akaketi akawa akiwafundisha.