John 8:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba cha hazina alipokuwa anafundisha hekaluni. Wala hakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alisema maneno haya alipokuwa anafundisha katika eneo la Hekalu, karibu na chumba ambamo sadaka za Hekaluni zilitunzwa. Hata hivyo hakuna hata mmoja aliyemkamata, kwa sababu wakati sahihi wa kufanya hivyo ulikuwa bado haujafika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba cha hazina alipokuwa anafundisha Hekaluni. Wala hakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba cha hazina alipokuwa anafundisha hekaluni. Wala hakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia. Yesu akasema, “ ‘Niendako mimi ninyi hamwezi kufika.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba cha hazina alipokuwa anafundisha hekaluni. Wala hakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maneno haya aliyasema penye sanduku ya vipaji alipofundishia Patakatifu. Lakini hata mmoja hakumkamata, kwani saa yake ilikuwa haijafika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alisema maneno haya wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, kwenye sanduku za kuwekea matoleo. Hakuna mutu aliyemufunga, kwa sababu wakati wake ulikuwa haujatimia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maneno haya aliyasema Yesu akifundisha kakika hekalu, katika chumba cha hazina; wala hapana mtu aliyemkamata, kwa kuwa saa yake ilikuwa haijaja bado.