John 8:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawaambia tena, “Naenda zangu nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, nyinyi hamwezi kufika.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kuja.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa mara nyingine, Yesu akawaambia watu, “Mimi nitawaacha. Nanyi mtanitafuta, lakini pamoja na hayo mtakufa katika dhambi zenu. Kwani hamuwezi kuja kule niendako.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawaambia tena, “Naenda zangu nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kufika.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawaambia tena, “Naenda zangu nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, nyinyi hamwezi kufika.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako ninyi hamwezi kuja.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi ninyi hamwezi kuja.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamuwezi kuja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawaambia tena, “Naenda zangu nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, nyinyi hamwezi kufika.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia tena: Mimi nakwenda zangu, nanyi mtanitafuta, hata kufa mtakufa, mko katika ukosaji wenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kukufika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaambia watu tena: “Mimi ninajiendea, nanyi mutanitafuta, lakini mutakufa katika zambi zenu. Na zaidi ya hii hamuwezi kufika pahali ninapokwenda.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Yesu akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta, na mtakufa katika dhambi yenu: niendako mimi, ninyi hamwezi kuja.