John 8:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wakamjibu, “Sisi ni wazawa wa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: ‘Mtakuwa huru?’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Ibrahimu, nasi hatujakuwa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakamjibu, “Sisi ni wazaliwa wa Ibrahimu. Na hatujawahi kamwe kuwa watumwa. Sasa kwa nini unasema kuwa tutapata uhuru?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nao wakamjibu, “Sisi ni wazawa wa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: mtakuwa huru?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wakamjibu, “Sisi ni wazawa wa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: ‘Mtakuwa huru?’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu ye yote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Ibrahimu, nasi hatujawa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Abrahamu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wowote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wakamjibu, “Sisi ni wazawa wa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: ‘Mtakuwa huru?’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamjibu: Sisi tu uzao wake Aburahamu, hatujawa bado watumwa wa mtu, nawe wasemaje: Mtakombolewa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu: “Sisi ni wa uzao wa Abrahamu, wala hatujakuwa watumwa wa mutu hata siku moja. Namna gani basi unaweza kutuambia kwamba tutapata uhuru?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamjihu, Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wanenaje, Mtawekwa huru?