John 8:37 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Najua kwamba nyinyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamyakubali mafundisho yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Ibrahimu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Najua kuwa ninyi ni wazaliwa wa Ibrahimu. Lakini mmekusudia kuniua, kwa sababu hamtaki kuyakubali mafundisho yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Najua kwamba ninyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamuyakubali mafundisho yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Najua kwamba nyinyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamyakubali mafundisho yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Abrahamu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Ibrahimu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Abrahamu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Najua kwamba nyinyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamyakubali mafundisho yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninajua, ya kuwa ninyi m uzao wake Aburahamu. Lakini mnatafuta kuniua, kwani ndani yenu Neno langu halipati pa kukaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninajua kwamba ninyi ni uzao wa Abrahamu. Lakini munatafuta kuniua, kwa sababu munakataa kukubali mafundisho yangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.