John 8:40 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, nyinyi mwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya jambo la namna hii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mimi ni mtu niliyewaambia ukweli niliousikia kutoka kwa Mungu. Lakini Ibrahimu hakufanya kama hayo mnayotaka kufanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, ninyi mwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, nyinyi mwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu, Abrahamu hakufanya jambo la namna hii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu, Ibrahimu hakufanya jambo la namna hii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Abrahamu hakufanya hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, nyinyi mwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa mnatafuta kuniua; nami nimewaambia iliyo ya kweli, niliyoisikia kwa Mungu; hivyo Aburahamu hakuvifanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa munatafuta kuniua ijapokuwa nimewaambia ukweli niliousikia kutoka kwa Mungu. Abrahamu hakufanya vile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu niliyewaambia kweli ile niliyoisikia kwa Baba yangu. Ibrahimu hakufanya hivi. Ninyi nmazitenda kazi za baba yenu.