John 8:53 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, unajifanya mkuu kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa, na manabii ambao pia walikufa? Unafikiri wewe ni nani?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wewe si mkuu zaidi ya baba yetu Ibrahimu! Yeye alikufa na manabii nao walikufa. Unadhani wewe ni nani?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, unajifanya mkuu kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa na manabii ambao nao pia walikufa? Hivi wewe unajifanya kuwa nani?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa na manabii ambao nao pia walikufa? Hivi wewe unajifanya kuwa nani?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe u mkuu kuliko baba yetu Abrahamu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, unajifanya mkuu kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Wewe u mkubwa kuliko baba yetu Aburahamu aliyekufa? Nao wafumbuaji wamekufa. Wajifanya kuwa nani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe ni mukubwa kuliko babu yetu Abrahamu? Yeye alikufa, na manabii walikufa vilevile. Wewe unajiona kuwa nani?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, nae amekufa? Na manabii wamekufa; wajifanya kuwa nani?