John 8:55 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama nyinyi. Mimi namjua na ninashika neno lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kwa hakika hamumjui yeye. Mimi namjua. Kama ningesema simjui, basi ningekuwa mwongo kama ninyi. Lakini namjua, na kuyatii anayosema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namjua na ninashika neno lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama nyinyi. Mimi namjua na ninashika neno lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama nyinyi. Mimi namjua na ninashika neno lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi hamkumtambua yeye, lakini mimi nimemjua. Nami kama ningesema: Simjui, ningefanana nanyi kuwa mwongo. Lakini nimemjua, nalo Neno lake ninalishika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi hamumujui, lakini mimi ninamujua. Kama ningesema kwamba simujui, ningekuwa mwongo kama ninyi. Lakini ninamujua na ninashika neno lake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nanyi hamkumjua; lakini mimi namjua, na nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua na neno lake nalishika.