John 8:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Isa akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hao waliyasema haya ili kumtega Yesu. Walitaka kumkamata akisema mambo tofauti ili wapate mashtaka ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama chini na kuanza kuandika kwenye udongo kwa kidole chake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walimwuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Isa akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walisema hivyo kwa kumjaribu, wapate neno la kumsuta. Yesu akainama chini, akaandika mchangani kwa kidole.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao walisema hivi kwa kumupima, kusudi wapate sababu ya kumushitaki. Lakini Yesu akainama na kuandika juu ya udongo kwa kidole chake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakasema neno hili wakimjaribu wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika inchi.