John 8:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Viongozi wa Kiyahudi waliendelea kumuuliza swali lao hilo. Naye akainuka na kusema, “Yeyote hapa ambaye hajawahi kutenda dhambi awe wa kwanza kumponda jiwe mwanamke huyu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu ye yote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipozidi kumhoji, aliinuka, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, “Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walipokaza kumwuliza, akainua macho, akawaambia: Ninyi, asiye na kosa na aanze kumtupia jiwe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka na kuwaambia: “Mutu asiyekuwa na zambi kati yenu, akuwe wa kwanza kumutupia jiwe.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wakazidi kumhoji, akajiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

Recommended Reading