John 9:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, “Maadamu yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?” Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho. Wasemaje kuhusu mtu huyo?” Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakamuuliza tena huyo mtu, “Kwa vile aliponya macho yako, unasemaje juu ya mtu huyo?” Akajibu, “Yeye ni nabii.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, “Maadam yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?” Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, “Maadamu yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?” Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho, wasemaje kuhusu mtu huyo?” Maana macho yako ndiyo yaliyofumbuliwa. Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho, wasemaje kuhusu mtu huyo?” Maana macho yako ndiyo yaliyofumbuliwa. Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje kuhusu habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, “Maadamu yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?” Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wakamwambia kipofu tena: Wewe unamwona kuwa nani, kwa sababu alikufumbua macho? Naye akasema: Ni mfumbuaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafarisayo wakamwuliza tena yule aliyekuwa kipofu: “Na wewe unasema nini juu ya yule aliyekuponyesha macho?” Akajibu: “Yeye ni nabii.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kukawa matangukano kati yao. Bassi wakamwambia yule kipofu marra ya pili, Wewe unasema nini katika khabari zake kwa kuwa alikufumbua macho? Akasema, Yu nabii.