John 9:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi, kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Isa kuwa ndiye Al-Masihi atafukuzwa kutoka sinagogi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walisema hivi kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Kiyahudi. Viongozi walikwisha azimia kwamba, wangemwadhibu mtu yeyote ambaye angesema Yesu alikuwa Masihi. Wangewazuia hao wasije tena kwenye sinagogi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa Wayahudi kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu ye yote atakayemkiri Yesu kuwa ndiye Kristo atafukuzwa kutoka katika sinagogi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa Wayahudi kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Isa kuwa ndiye Al-Masihi atafukuzwa kutoka sinagogi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kukubaliana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wazazi wake walisema hivyo kwa kuwaogopa Wayuda, kwani Wayuda walikuwa wamekula njama ya kwamba: Mtu atakayemwungama, kuwa ni Kristo, akatazwe kuiingia nyumba ya kuombea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliogopa wakubwa wa Wayuda. Wakubwa wale walikuwa wamekwisha kupatana kwamba mutu yeyote anayesadiki kuwa Yesu ndiye Kristo, atatengwa asiingie katika nyumba ya kuabudia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wazazi wake waliyasema haya kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi wamekwisha kuwafikana kwamba mtu akimwungama kuwa Kristo, ataharamishwa sunagogi.