John 9:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakamwita tena huyo aliyekuwa kipofu, wakamwambia, “Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo viongozi wa Kiyahudi wakamwita yule aliyekuwa haoni. Wakamwambia aingie ndani tena. Wakasema, “Unapaswa kumheshimu Mungu na kutuambia ukweli. Tunamjua mtu huyu kuwa ni mtenda dhambi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakamwita tena aliyekuwa kipofu, wakamwambia, “Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakamwita tena huyo aliyekuwa kipofu, wakamwambia, “Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakamwita tena huyo aliyekuwa kipofu, wakamwambia, “Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kisha wakamwita mara ya pili yule mtu aliyekuwa ni kipofu, wakamwambia: Mtukuze Mungu! Sisi twajua: Mtu huyo ni mkosaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakubwa wa Wayuda wakamwita yule aliyekuwa kipofu kwa mara ya pili na kumwambia: “Sema ukweli mbele ya Mungu! Kwa ngambo yetu tunajua kwamba mutu yule ni mwenye zambi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi marra ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.