John 9:35 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuza sunagogini. Basi, alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa aliposikia kuwa wamemfukuza atoke nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta, akamuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliposikia kuwa walimlazimisha huyo mtu kuondoka, alikutana naye na kumuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuzia mbali, naye alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuza sunagogini. Basi, alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu aliposikia kuwa wamemfukuzia nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta akamwuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa aliposikia kuwa wamemfukuzia nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta akamuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuza sunagogini. Basi, alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akasikia, ya kuwa wamemfukuza, atoke; alipomwona akasema: Unamtegemea Mwana wa mtu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akapata habari kwamba yule aliyekuwa kipofu amefukuzwa. Yesu alipokutana naye, akamwuliza: “Unamwamini Mwana wa Mutu?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; akamwona, akasema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?