John 9:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kukiwa bado ni mchana, tunapaswa kuendelea kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma. Usiku unakuja, na hakuna mtu atakayeweza kufanya kazi wakati wa usiku.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Imenipasa kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sisi sharti tuzifanye kazi zake aliyenituma, mchana ukingali upo. Usiku unakuja, pasipowezekana kufanya kazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Imetupasa kufanya kazi za yule aliyenituma wakati kungali muchana, kwa sababu usiku unakaribia, wakati mutu asipoweza kutumika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yanipasa kuzifanya kazi zake aliyenipeleka maadam ni mchana: usiku waja, asipoweza mtu kufanya kazi.