John 9:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Hapo, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu” (Siloamu maana yake ni Kutumwa). Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu” (Siloamu maana yake ni “Aliyetumwa”.) Hivyo mtu yule akaenda katika bwawa lile, akanawa na kurudi akiwa mwenye kuona.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Basi, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Hapo, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu, maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu, maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akamwambia, Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi akiwa anaona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Hapo, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamwambia: Nenda, unawe katika ziwa la Siloa, ni kwamba: Aliyetumwa. Basi, akaenda, akanawa, akarudi mwenye kuona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kumwambia: “Kwenda unawe uso katika kisima cha Siloamu” (maana ya jina hili ni “Aliyetumwa”). Basi yule kipofu akaenda na kunawa uso, akarudi akiwa mwenye kuona.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akampaka kipofu macho kwa lile tope, akamwambia, Enenda, kanawe katika birika ya Siloam (tafsiri yake, Aliyetumwa). Bassi akaenda, akanawa, akarudi, anaona.