Jonah 1:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakamlilia Mwenyezi-Mungu wakisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, twakusihi usituangamize kwa kuutoa uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa kumwaga damu ya mtu asiye na hatia. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, umefanya upendavyo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wakamlilia Mwenyezi Mungu, “Ee Mwenyezi Mungu, tafadhali usituue kwa kumuua mtu huyu. Usituhesabie hatia kwa kumuua mtu asiyekuwa na hatia, kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umefanya kama ilivyokupendeza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakamlilia Mwenyezi-Mungu wakisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, twakusihi usituangamize kwa kuutoa uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa kumwaga damu ya mtu asiye na hatia. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, umefanya upendavyo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wakamlilia BWANA, “Ee BWANA, tafadhali usituue kwa kuondoa uhai wa mtu huyu. Usituhesabie hatia kwa kuutoa uhai wa mtu asiyekuwa na hatia, kwa kuwa wewe Ee BWANA, umefanya kama ilivyokupendeza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wakamlilia bwana, “Ee bwana, tafadhali usituue kwa kuondoa uhai wa mtu huyu. Usituhesabie hatia kwa kuutoa uhai wa mtu asiyekuwa na hatia, kwa kuwa wewe, Ee bwana, umefanya kama ilivyokupendeza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakamlilia BWANA, wakasema, Twakuomba, Ee BWANA, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, BWANA, umefanya kama ulivyopenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakamlilia Mwenyezi-Mungu wakisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, twakusihi usituangamize kwa kuutoa uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa kumwaga damu ya mtu asiye na hatia. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, umefanya upendavyo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipomlilia Bwana kwamba: E Bwana, usiache, tukiangamia kwa ajili ya roho ya mtu huyu! Wala usitutwike damu, tusiyoikosea! Kwani wewe Bwana umefanya, kama ulivyopendezwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakamlilia BWANA, wakasema, Twakuomba, Ee BWANA, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, BWANA, umefanya kama ulivyopenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakamulilia Yawe wakisema: Ee Yawe, tunakusihi usituangamize kwa kuutoa uzima wa mutu huyu, wala usituazibu kwa kumwanga damu ya mutu asiyekuwa na kosa. Wewe, ee Yawe, umefanya unavyopenda.