Jonah 1:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mabaharia wakajawa na hofu, kila mmoja akaanza kumlilia mungu wake; wakatupa baharini shehena ya meli ili kupunguza uzito wake. Wakati huo, Yona alikuwa ameteremkia sehemu ya ndani ya meli, akawa amelala usingizi mzito.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito. Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mabaharia wakajawa na hofu, kila mmoja akaanza kumlilia mungu wake; wakatupa baharini shehena ya meli ili kupunguza uzito wake. Wakati huo, Yona alikuwa ameteremkia sehemu ya ndani ya meli, akawa amelala usingizi mzito.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito. Lakini Yona alikuwa ametelemkia chumba cha ndani ya meli, mahali ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito. Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, mahali ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hadi pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mabaharia wakajawa na hofu, kila mmoja akaanza kumlilia mungu wake; wakatupa baharini shehena ya meli ili kupunguza uzito wake. Wakati huo, Yona alikuwa ameteremkia sehemu ya ndani ya meli, akawa amelala usingizi mzito.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mabaharia wakaogopa, wakaililia miungu, kila mtu mungu wake, kisha vyombo vilivyokuwamo merikebuni wakavitupa baharini, merikebu ipate kuwa nyepesi. Lakini Yona alikuwa ameshuka na kuingia chumba cha ndani cha huko chini, akalala usingizi mwingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watumishi wa mashua wakaogopa, kila mumoja akaanza kumulilia mungu wake. Wakatupa katika bahari mizigo yote kwa kupunguza uzito wa mashua. Wakati ule, Yona alikuwa ameshuka katika sehemu ya ndani ya mashua, akalala usingizi muzito.