Jonah 2:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima, katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umenipandisha hai kutoka humo shimoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilizama chini sana hata pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima, katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umenipandisha hai kutoka humo shimoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee BWANA Mungu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima, katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umenipandisha hai kutoka humo shimoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maji yamenizunguka ya kuitosa nayo roho yangu, vilindi vimenizunguka, majani ya baharini yamekizinga kichwa changu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maji yalinizunguka na kunisonga; kilindi kilinifikia kila upande, majani ya bahari yakanifunika kichwa.