Jonah 3:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Habari hizi zikamfikia mfalme wa Ninewi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake rasmi, akajivika vazi la gunia na kuketi katika majivu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha utawala, akavua majoho yake ya mfalme, akajifunika gunia na kuketi mavumbini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Habari hizi zikamfikia mfalme wa Ninewi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake rasmi, akajivika vazi la gunia na kuketi katika majivu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Habari hizi zikamfikia mfalme wa Ninewi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake rasmi, akajivika vazi la gunia na kuketi katika majivu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Habari ya mambo hayo ikafika hata kwa mfalme wa Niniwe, naye akaondoka katika kiti chake cha kifalme, akalivua vazi lake la kifalme, akavaa gunia, akajikalisha majivuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Habari hizi zikamufikia mufalme wa Ninawe, naye akaondoka juu ya kiti chake cha kifalme, akavua nguo yake ya kifalme, akavaa gunia na kuikaa katika majivu.