Jonah 3:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme akawatangazia wakazi wa Ninewi: “Mimi mfalme, pamoja na wakuu wangu, natoa amri hii: Pasiwe na binadamu yeyote, ng'ombe au mnyama yeyote wa kufugwa, atakayeonja kitu chochote. Ni mwiko kwa mtu yeyote au mnyama kula au kunywa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote: “Kwa amri ya mfalme na wakuu wake: “Msiruhusu mtu yeyote au mnyama, makundi ya ng’ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu chochote, msiwaruhusu kula wala kunywa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme akawatangazia wakazi wa Ninewi: “Mimi mfalme, pamoja na wakuu wangu, natoa amri hii: Pasiwe na binadamu yeyote, ng'ombe au mnyama yeyote wa kufugwa, atakayeonja kitu chochote. Ni mwiko kwa mtu yeyote au mnyama kula au kunywa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote: “Kwa amri ya mfalme na wakuu wake: “Msiruhusu mtu ye yote au mnyama, makundi ya ng'ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu cho chote, msiwaruhusu kula wala kunywa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote: “Kwa amri ya mfalme na wakuu wake: “Msiruhusu mtu yeyote au mnyama, makundi ya ng’ombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu chochote, msiwaruhusu kula wala kunywa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme akawatangazia wakazi wa Ninewi: “Mimi mfalme, pamoja na wakuu wangu, natoa amri hii: Pasiwe na binadamu yeyote, ng'ombe au mnyama yeyote wa kufugwa, atakayeonja kitu chochote. Ni mwiko kwa mtu yeyote au mnyama kula au kunywa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatangaza mbiu mle Niniwe ya kwamba: Kwa amri ya mfalme na ya wakuu wake yanaagizwa haya: Watu na nyama, kama ni ng'ombe au kondoo, wasionje kitu cho chote, wasile, wala maji tu wasinywe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme akawatangazia wakaaji wa Ninawe: Mimi mufalme, pamoja na wakubwa wangu, ninatoa amri hii: Kusikuwe mutu yeyote, ngombe au nyama yeyote wa kufugwa, atakayeonja kitu chochote. Hairuhusiwi kwa mutu yeyote au nyama kula au kunywa.