Jonah 4:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, haifai kwangu kuuhurumia mji wa Ninewi, ule mji mkuu wenye watu 120,000, wasioweza kupambanua jema na baya, na pia wanyama wengi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Ninawi ina zaidi ya watu elfu mia moja na ishirini ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ng’ombe wengi. Je, hainipasi kufikiri kuhusu mji ule mkubwa?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, haifai kwangu kuuhurumia mji wa Ninewi, ule mji mkuu wenye watu 120,000, wasioweza kupambanua jema na baya, na pia wanyama wengi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto pamoja na ng'ombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ng’ombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya elfu mia moja na ishirini, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, haifai kwangu kuuhurumia mji wa Ninewi, ule mji mkuu wenye watu 120,000, wasioweza kupambanua jema na baya, na pia wanyama wengi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nisiuonee uchungu mji huu mkubwa wa Niniwe, kwa kuwa humu wamo watu kupita 120000 wasiojua kupambanua yaliyoko kuumeni nayo yaliyoko kushotoni? Tena wamo nyama wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, haifai kwangu kuuhurumia Ninawe, ule muji mukubwa wenye watu elfu mia moja na makumi mbili, wasioweza kutambua linalokuwa jema na baya; na nyama wengi wasiokuwa na hesabu?