Jonah 4:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo akaomba, “Mwenyezi-Mungu, je, hayo si mambo yaleyale niliyowaza utayafanya nilipokuwa nyumbani? Ndio maana nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi. Nilijua kwamba wewe u Mungu wa upendo na huruma. Hukasiriki upesi, daima u mwema na u tayari kubadili nia yako wakati wowote ili usiadhibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwomba Mwenyezi Mungu, “Ee Mwenyezi Mungu, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharakisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwomba Bwana, akasema, Nakuomba, Ee Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo akaomba, “Mwenyezi-Mungu, je, hayo si mambo yaleyale niliyowaza utayafanya nilipokuwa nyumbani? Ndio maana nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi. Nilijua kwamba wewe u Mungu wa upendo na huruma. Hukasiriki upesi, daima u mwema na u tayari kubadili nia yako wakati wowote ili usiadhibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwomba BWANA, “Ee BWANA, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwomba bwana, “Ee bwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nilijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo akaomba, “Mwenyezi-Mungu, je, hayo si mambo yaleyale niliyowaza utayafanya nilipokuwa nyumbani? Ndio maana nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi. Nilijua kwamba wewe u Mungu wa upendo na huruma. Hukasiriki upesi, daima u mwema na u tayari kubadili nia yako wakati wowote ili usiadhibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamwomba Bwana kwamba: E Bwana, haya siyo, niliyoyasema nilipokuwa katika nchi ya kwetu? Kwa hiyo naliondoka kukimbilia Tarsisi, kwani nalijua, ya kuwa wewe ndiwe Mungu mwenye utu na huruma, tena u mwenye uvumilivu na upole mwingi, hugeuza moyo, usifanye mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwomba BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo akaomba: Yawe, si hayo ndiyo mambo yaleyale niliyowaza utayafanya nilipokuwa katika inchi yangu? Ndiyo maana nilifanya haraka kukimbilia Tarsisi. Nilijua kwamba wewe ni Mungu ambaye umejaa huruma na rehema, haukasiriki upesi, wewe ni mwingi wa wema, na tayari kubadilisha nia yako kusudi usiazibu.