Jonah 4:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Yona akatoka nje ya mji, akajikalia upande wa mashariki wa mji huo. Hapo, akajijengea kibanda, akaketi kivulini mwake huku anangojea apate kuona litakaloupata mji wa Ninewi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule utakuwaje.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Yona akatoka nje ya mji, akajikalia upande wa mashariki wa mji huo. Hapo, akajijengea kibanda, akaketi kivulini mwake huku anangojea apate kuona litakaloupata mji wa Ninewi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajitengenezea kibanda huko, akakaa chini yake kivulini, hadi aone mji ule utakuwaje.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Yona akatoka nje ya mji, akajikalia upande wa mashariki wa mji huo. Hapo, akajijengea kibanda, akaketi kivulini mwake huku anangojea apate kuona litakaloupata mji wa Ninewi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yona akatoka mle mjini, akakaa nje ya mji upande wa maawioni kwa jua, akajijengea kibanda kidogo, akakaa chini yake kivulini, mpaka aone, mambo ya mji yatakavyokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule utakuwaje.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yona akatoka inje ya muji, akajiikalia upande wa mashariki wa muji huo. Pale, akajijengea kibanda, akaikaa chini ya kivuli chake akingojea apate kuona jambo litakaloupata muji wa Ninawe.