Jonah 4:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jua lilipochomoza, Mungu akaleta upepo wa hari kutoka mashariki, jua likamchoma sana Yona kichwani, karibu azirai. Yona akasema, “Afadhali kufa kuliko kuishi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona hadi akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jua lilipochomoza, Mungu akaleta upepo wa hari kutoka mashariki, jua likamchoma sana Yona kichwani, karibu azirai. Yona akasema, “Afadhali kufa kuliko kuishi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akatayarisha upepo wa mashariki, wenye joto jingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jua lilipochomoza, Mungu akaleta upepo wa hari kutoka mashariki, jua likamchoma sana Yona kichwani, karibu azirai. Yona akasema, “Afadhali kufa kuliko kuishi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaagiza upepo wenye joto utokao upande wa maawioni kwa jua; basi, jua lilipompiga Yona kichwani, akazimia, akajitakia kufa akisema: Kufa kwangu ni kwema kuliko kuishi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jua lilipotokea, Mungu akaleta upepo mukali kutoka upande wa jangwa, jua likamuchoma sana Yona juu ya kichwa, karibu azimie. Akatamani kufa, akisema: Ni vizuri kwangu kufa kuliko kuishi.