Joshua 1:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Piteni katika kambi na kuwaamrisha watu watayarishe chakula, kwa kuwa baada ya siku tatu mtavuka mto Yordani, kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawapeni iwe mali yenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Tayarisheni vyakula vyenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa iwe yenu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wenu, mpate kuimiliki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Piteni katika kambi na kuwaamrisha watu watayarishe chakula, kwa kuwa baada ya siku tatu mtavuka mto Yordani, kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawapeni iwe mali yenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Wekeni tayari mahitaji yenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka hii Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo BWANA Mungu wenu anawapa iwe yenu wenyewe.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Wekeni tayari mahitaji yenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka hii Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa iwe yenu wenyewe.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Piteni katika kambi, mkawaamuru hao watu, mkisema, Tayarisheni vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Piteni katika kambi na kuwaamrisha watu watayarishe chakula, kwa kuwa baada ya siku tatu mtavuka mto Yordani, kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawapeni iwe mali yenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Piteni makambini po pote, mwaagize watu kwamba: Jitengenezeeni pamba za njiani! Kwani baada ya siku tatu mtauvuka huu Yordani kwenda kuichukua hiyo nchi, Bwana Mungu wenu atakayowapa ninyi, mwichukue, iwe yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mupite katika kambi na kuwaamuru watu watayarishe chakula, kwa sababu kisha siku tatu mutavuka muto Yordani, kwenda kuirizi inchi ambayo Yawe, Mungu wenu, anawapa ikuwe mali yenu.”