Joshua 1:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wake zenu, watoto wenu na wanyama wenu wa kufugwa watabaki katika nchi hiyo ambayo Mose aliwapeni, ngambo ya mto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka mto na kuwatangulia ndugu zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ambayo Musa aliwapa mashariki mwa Yordani, lakini wapiganaji wenu wote, wakiwa wamejiandaa kwa vita, lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wake zenu, na watoto wenu, na makundi yenu, watakaa katika nchi aliyowapa Musa ng'ambo ya Yordani; bali ninyi mtavuka mbele ya ndugu zenu, hali mmevikwa silaha zenu, watu wote wenye nguvu, na ushujaa, ili mpate kuwasaidia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wake zenu, watoto wenu na wanyama wenu wa kufugwa watabaki katika nchi hiyo ambayo Mose aliwapeni, ng'ambo ya mto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka mto na kuwatangulia ndugu zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ile Mose aliyowapa mashariki ya Yordani, lakini mashujaa wenu wote, wakiwa wamevikwa silaha kikamilifu lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu hadi
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ile Musa aliyowapa mashariki ya Yordani, lakini mashujaa wenu wote, wakiwa wamevikwa silaha kikamilifu lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu hadi
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wake zenu, na watoto wenu, na makundi yenu, watakaa katika nchi aliyowapa Musa ng'ambo ya Yordani; bali ninyi mtawatangulia ndugu zenu kuvuka, mkiwa mmevaa silaha zenu, watu wote wenye nguvu, na ushujaa, ili mpate kuwasaidia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wake zenu, watoto wenu na wanyama wenu wa kufugwa watabaki katika nchi hiyo ambayo Mose aliwapeni, ngambo ya mto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka mto na kuwatangulia ndugu zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wake na watoto na nyama wenu wa kufuga watakaa katika nchi hii, Mose aliyowapa ninyi ng'ambo hii ya Yordani; lakini ninyi nyote mlio mafundi wa vita wenye nguvu mtashika mata, mvuke na kuwatangulia ndugu zenu, mwasaidie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wake zenu, na watoto wenu, na makundi yenu, watakaa katika nchi aliyowapa Musa ng’ambo ya Yordani; bali ninyi mtavuka mbele ya ndugu zenu, hali mmevikwa silaha zenu, watu wote wenye nguvu, na ushujaa, ili mpate kuwasaidia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wake zenu, watoto wenu na nyama wenu wa kufugwa watabaki katika inchi hiyo ambayo Musa aliwapa, ngambo ya muto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka muto na kuwatangulia wandugu zenu.