Joshua 1:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtawasaidia mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowapa ndugu zenu pia mahali pa kupumzikia, kama alivyowapa nyinyi, nao pia wamiliki nchi ambayo wanapewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kisha mtarudi katika nchi ambayo ni mali yenu na kuimiliki, nchi ambayo mlipewa na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, mashariki ya mto Yordani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hadi Mwenyezi Mungu awape nao utulivu, kama alivyowatendea ninyi, hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kuimiliki nchi yenu wenyewe, ambayo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata Bwana atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Bwana aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtawasaidia mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowapa ndugu zenu pia mahali pa kupumzikia, kama alivyowapa nyinyi, nao pia wamiliki nchi ambayo wanapewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kisha mtarudi katika nchi ambayo ni mali yenu na kuimiliki, nchi ambayo mlipewa na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, mashariki ya mto Yordani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA awape nao raha, kama alivyokwisha kufanya kwa ajili yenu hadi wao nao watakapokuwa wamemiliki nchi ile BWANA Mungu wenu anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kukalia nchi yenu wenyewe, ambayo Mose mtumishi wa BWANA aliwapa mashariki ya Yordani kuelekea linakochomoza jua.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana awape nao raha, kama alivyokwisha kufanya kwa ajili yenu hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile bwana Mwenyezi Mungu wenu anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kukalia nchi yenu wenyewe, ambayo Musa mtumishi wa bwana aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hadi BWANA atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wapate kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa mawio ya jua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtawasaidia mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowapa ndugu zenu pia mahali pa kupumzikia, kama alivyowapa nyinyi, nao pia wamiliki nchi ambayo wanapewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kisha mtarudi katika nchi ambayo ni mali yenu na kuimiliki, nchi ambayo mlipewa na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, mashariki ya mto Yordani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena hapo, Bwana atakapowapatia nao ndugu zenu kutulia kama ninyi, nao waichukue hiyo nchi, Bwana Mungu wenu watakavyowapa, iwe yao, ndipo, mtakaporudi katika nchi iliyo yenu wenyewe, mwichukue, iwe yenu kweli, ni hii, Mose, mtumishi wa Bwana, aliyowapa ninyi ng'ambo hii ya Yordani upande wa maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata BWANA atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwapeni ng’ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutawasaidia mpaka Yawe atakapowapa wandugu zenu vilevile pahali pa kupumzika, kama vile alivyowapa ninyi, nao vilevile warizi inchi ambayo wanapewa na Yawe, Mungu wenu. Kisha mutarudi katika inchi ambayo ni mali yenu na kuirizi, inchi ambayo mulipewa na Musa, mutumishi wa Yawe, ngambo ya muto Yordani.”