Joshua 1:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mipaka ya nchi yenu itakuwa hivi: Kusini ni jangwa, kaskazini ni milima ya Lebanoni, mashariki ni mto ule mkubwa Eufrate, kupitia nchi yote ya Wahiti hadi bahari ya Mediteranea upande wa magharibi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa iliyo upande wa magharibi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mipaka ya nchi yenu itakuwa hivi: kusini ni jangwa, kaskazini ni milima ya Lebanoni, mashariki ni mto ule mkubwa Eufrate, kupitia nchi yote ya Wahiti hadi bahari ya Mediteranea upande wa magharibi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto huu mkubwa wa Eufrati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa iliyoko upande wa magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa iliyoko upande wa magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Toka jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mipaka ya nchi yenu itakuwa hivi: Kusini ni jangwa, kaskazini ni milima ya Lebanoni, mashariki ni mto ule mkubwa Eufrate, kupitia nchi yote ya Wahiti hadi bahari ya Mediteranea upande wa magharibi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kutoka nyikani na huko Libanoni mpaka kwenye lile jito kubwa, lile jito la Furati, nchi yote nzima ya Wahiti, tena mpaka kwenye Bahari Kubwa iliyoko upande wa machweoni kwa jua; huko ndiko, mpaka wenu utakakokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mipaka ya inchi yenu itakuwa hivi: upande wa kusini ni jangwa, kaskazini ni milima ya Lebanoni, mashariki ni muto ule mukubwa Furati, kupitia inchi yote ya Wahiti mpaka bahari ya Mediteranea upande wa magaribi.