Joshua 1:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ila tu, uwe imara na hodari; uwe mwangalifu na kuzingatia sheria yote aliyokuamuru mtumishi wangu Mose. Fuata kila sehemu ya sheria hiyo nawe utafanikiwa popote uendapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Musa mtumishi wangu; usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote utakapoenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ila tu, uwe imara na hodari; uwe mwangalifu na kuzingatia sheria yote aliyokuamuru mtumishi wangu Mose. Fuata kila sehemu ya sheria hiyo nawe utafanikiwa popote uendapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria zote alizokupa Mose mtumishi wangu, usiziache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa po pote uendako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Musa mtumishi wangu, usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote uendako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ila tu, uwe imara na hodari; uwe mwangalifu na kuzingatia sheria yote aliyokuamuru mtumishi wangu Mose. Fuata kila sehemu ya sheria hiyo nawe utafanikiwa popote uendapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni hii tu: Jipe moyo, upate nguvu sana za kuyaangalia na kuyafanya Maonyo yote, mtumishi wangu Mose aliyokuagiza! Usiyaache kupitia kuumeni wala kushotoni, upate kujua njia ya kweli po pote, utakapokwenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukuwe tu imara na hodari. Ukuwe mwangalifu na kushika sheria yote mutumishi wangu Musa aliyokuamuru. Fuata kila sehemu ya sheria hiyo nawe utafanikiwa popote utakapoenda.