Joshua 1:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakikisha kuwa hutakisahau kamwe kitabu hiki cha sheria; bali kila siku utajifunza kitabu hiki, mchana na usiku, ili upate kutekeleza yote yaliyoandikwa humu, nawe utafanikiwa na kustawi popote uendapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakikisha kuwa hutakisahau kamwe kitabu hiki cha sheria; bali kila siku utajifunza kitabu hiki, mchana na usiku, ili upate kutekeleza yote yaliyoandikwa humu, nawe utafanikiwa na kustawi popote uendapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapoifanikisha njia yako na kisha utastawi sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakikisha kuwa hutakisahau kamwe kitabu hiki cha sheria; bali kila siku utajifunza kitabu hiki, mchana na usiku, ili upate kutekeleza yote yaliyoandikwa humu, nawe utafanikiwa na kustawi popote uendapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kitabu cha Maonyo haya kisiondoke kinywani mwako, ila uyawaze moyoni mchana na usiku, upate kuyaangalia na kuyafanya yote yaliyoandikiwa humo, kwani ndivyo, utakavyofanikiwa katika njia zako kwa kuzijua zitakazokuwa za kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakikisha kwamba hautakisahau hata kidogo kitabu hiki cha sheria; lakini kila siku utajifunza kitabu hiki, muchana na usiku, kusudi upate kutimiza yote yaliyoandikwa humu, nawe utastawi na kufanikiwa.