Joshua 10:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Mwenyezi-Mungu alipowatia Waamori mikononi mwa Waisraeli, Yoshua alimwomba Mwenyezi-Mungu mbele ya Waisraeli wote, akasema, “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, katika bonde la Aiyaloni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ile Mwenyezi Mungu alipowakabidhi Waamori kwa Waisraeli, Yoshua akanena na Mwenyezi Mungu akiwa mbele ya Waisraeli, akasema: “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Mwenyezi-Mungu alipowatia Waamori mikononi mwa Waisraeli, Yoshua alimwomba Mwenyezi-Mungu mbele ya Waisraeli wote, akasema, “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, katika bonde la Aiyaloni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ile ambayo BWANA aliwatia Waamori mikononi mwa Israeli, Yoshua akasema na BWANA mbele ya Waisraeli: “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, simama katika Bonde la Aiyaloni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ile ambayo bwana aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na bwana akiwa mbele ya Waisraeli akasema: “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Mwenyezi-Mungu alipowatia Waamori mikononi mwa Waisraeli, Yoshua alimwomba Mwenyezi-Mungu mbele ya Waisraeli wote, akasema, “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, katika bonde la Aiyaloni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo, Bwana alipowatoa Waamori machoni pa wana wa Isiraeli, ndipo, Yosua alipomwomba Bwana akisema masikioni pa Waisiraeli: Jua, simama kimya huko Gibeoni! Nawe mwezi, bondeni kwa Ayaloni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Yawe alipowatia Waamori katika mikono ya Waisraeli, Yoshua alimwomba Yawe mbele ya Waisraeli wote, akasema: “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, katika bonde la Ayaloni.”