Joshua 10:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jua likasimama kimya na mwezi ukasimama mpaka taifa la Israeli lilipolipiza kisasi maadui wake. Kama alivyoandika katika kitabu cha Yashari, jua lilisimama kimya katikati ya mbingu, likakatiza safari yake ya kwenda kutua kwa siku nzima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo jua likasimama, nao mwezi ukatulia, hadi taifa hilo lilipokwisha kujilipizia kisasi kwa adui zake, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari. Jua likasimama katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku nzima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jua likasimama kimya na mwezi ukasimama mpaka taifa la Israeli lilipolipiza kisasi maadui wake. Kama alivyoandika katika kitabu cha Yashari, jua lilisimama kimya katikati ya mbingu, likakatiza safari yake ya kwenda kutua kwa siku nzima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo jua likasimama kimya, nao mwezi ukatulia, hadi Waisraeli walipokwisha kujipatilizia kwa adui zao, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari. Jua likasimama katikati ya mbingu kimya, likachelewa kuzama muda wa siku moja nzima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo jua likasimama, nao mwezi ukatulia, hadi taifa hilo lilipokwisha kujilipizia kisasi kwa adui wake, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari. Jua likasimama kimya katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku moja nzima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hadi hilo taifa lilipokuwa limekwisha jilipiza kisasi juu ya adui zao. Hayo, je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jua likasimama kimya na mwezi ukasimama mpaka taifa la Israeli lilipolipiza kisasi maadui wake. Kama alivyoandika katika kitabu cha Yashari, jua lilisimama kimya katikati ya mbingu, likakatiza safari yake ya kwenda kutua kwa siku nzima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, jua liliposimama kimya, nao mwezi ukasimama, hata watu wawalipize adui zao. Kumbe haya hayakuandikwa katika kitabu cha Mnyofu? Basi, jua likasimama katikati ya mbinguni, lisijihimize kuchwa muda kama wa siku nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. Hayo, je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jua likasimama kimya na mwezi ukasimama mpaka taifa la Israeli lilipolipiza kisasi waadui zake. Kama vile ilivyoandikwa katika kitabu cha Yaseri, jua lilisimama kimya katikati ya mbingu, likakatiza safari yake ya kwenda kutua kwa siku nzima.