Joshua 10:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku kama hiyo haijawahi kuwako kamwe wala haijapata kuonekana tena, siku ambayo Mwenyezi-Mungu amemwitikia binadamu kwa namna hiyo; maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwapigania Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakujakuwa na siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo Mwenyezi Mungu alimsikiliza mwanadamu. Hakika Mwenyezi Mungu alikuwa akiwapigania Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama baada yake, hata ikawa yeye Bwana kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa Bwana alipiga vita kwa ajili ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku kama hiyo haijawahi kuwako kamwe wala haijapata kuonekana tena, siku ambayo Mwenyezi-Mungu amemwitikia binadamu kwa namna hiyo; maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwapigania Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haijakuwepo siku nyingine mfano wa hiyo kabla au baada, siku ambayo BWANA alimsikiliza mwanadamu. Hakika BWANA alikuwa akiwapigania Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haijakuwepo siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo bwana alimsikiliza mwanadamu. Hakika bwana alikuwa akiwapigania Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizofuata baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku kama hiyo haijawahi kuwako kamwe wala haijapata kuonekana tena, siku ambayo Mwenyezi-Mungu amemwitikia binadamu kwa namna hiyo; maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwapigania Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ndefu kama hiyo haikuwa mbele yake wala nyuma yake, Bwana alipoisikia sauti ya mtu wake, kwani ndivyo, Bwana alivyowagombea Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakujakuwa siku kama hiyo hata kidogo wala haijapata kuonekana tena, siku ambayo Yawe amemwitikia mwanadamu kwa namna hiyo; maana Yawe mwenyewe aliwapigania Waisraeli.