Joshua 10:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafalme hao walipoletwa, Yoshua akawaita Waisraeli wote na wakuu wa majeshi waliokwenda naye vitani, akawaambia, “Njoni karibu mwakanyage wafalme hawa shingoni mwao.” Nao wakasogea na kuwakanyaga shingoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa wamewaleta hawa wafalme kwa Yoshua, akawaita wanaume wote wa Israeli, na kuwaambia majemadari wa vita walioenda pamoja naye, “Njooni hapa mweke nyayo zenu juu ya shingo za hawa wafalme.” Basi wakaja wakaweka nyayo zao shingoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafalme hao walipoletwa, Yoshua akawaita Waisraeli wote na wakuu wa majeshi waliokwenda naye vitani, akawaambia, “Njoni karibu mwakanyage wafalme hawa shingoni mwao.” Nao wakasogea na kuwakanyaga shingoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kuwaleta kwa Yoshua, akawaita watu wote wa Israeli, na kuwaambia majemadari wa vita waliokwenda pamoja naye, “Njoni hapa mweke nyayo zenu juu ya shingo za hawa wafalme.” Basi wakaja wakawakanyaga shingoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokuwa wamewaleta hawa wafalme kwa Yoshua, akawaita watu wote wa Israeli, na kuwaambia majemadari wa vita waliokwenda pamoja naye, “Njooni hapa mweke nyayo zenu juu ya shingo za hawa wafalme.” Basi wakaja wakaweka nyayo zao shingoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafalme hao walipoletwa, Yoshua akawaita Waisraeli wote na wakuu wa majeshi waliokwenda naye vitani, akawaambia, “Njoni karibu mwakanyage wafalme hawa shingoni mwao.” Nao wakasogea na kuwakanyaga shingoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, walipowatoa hawa wafalme na kuwapeleka kwa Yosua, Yosua akawaita Waisiraeli wote, akawaambia wakuu wa wapiga vita waliokwenda naye: Karibuni, mwiweke miguu yenu juu ya kosi za wafalme hawa! Ndipo, walipowakaribia, wakaiweka miguu yao juu ya kosi zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafalme hao walipoletwa, Yoshua akawaita Waisraeli wote na wakubwa wa waaskari waliokwenda naye kwa vita, akawaambia: “Mukuje karibu muwakanyage wafalme hawa kwenye shingo yao.” Nao wakasogea na kuwakanyaga kwenye shingo.