Joshua 10:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua akawaambia “Msiogope, wala msiwe na wasiwasi, muwe imara na hodari, maana hivi ndivyo Mwenyezi-Mungu atakavyowatendea adui zenu ambao mtapigana nao. Kwa hiyo, muwe imara na hodari.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoshua akawaambia, “Msiogope, wala msivunjike moyo. Kuweni hodari na wenye ushujaa. Hili ndilo Mwenyezi Mungu atakalowatendea adui zenu wote mnaoenda kupigana nao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua akawaambia, Msiche, wala msifadhaike; iweni hodari na wa mioyo ya ushujaa; kwa kuwa ndivyo Bwana atakavyowafanyia adui zenu wote ambao mwapigana nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua akawaambia “Msiogope, wala msiwe na wasiwasi, muwe imara na hodari, maana hivi ndivyo Mwenyezi-Mungu atakavyowatendea adui zenu ambao mtapigana nao. Kwa hiyo, muwe imara na hodari.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akawaambia, “Msiogope, wala msivunjike moyo. Iweni hodari na wenye moyo mkuu. Hili ndilo BWANA atakalowatendea adui zenu wote mnaokwenda kupigana nao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoshua akawaambia, “Msiogope, wala msivunjike moyo. Kuweni hodari na wenye ushujaa. Hili ndilo bwana atakalowatendea adui zenu wote mnaokwenda kupigana nao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua akawaambia, Msiogope, wala msifadhaike; iweni hodari na wa moyo wa ushujaa; kwa kuwa ndivyo BWANA atakavyowafanyia adui zenu wote ambao mnapigana nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua akawaambia “Msiogope, wala msiwe na wasiwasi, muwe imara na hodari, maana hivi ndivyo Mwenyezi-Mungu atakavyowatendea adui zenu ambao mtapigana nao. Kwa hiyo, muwe imara na hodari.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yosua akawaambia: Msiogope, wala msiingiwe na vituko! Jipeni mioyo, mpate nguvu! Kwani hivyo ndivyo, Bwana atakavyowafanyizia adui zenu wote, mtakapopigana nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua akawaambia, Msiche, wala msifadhaike; iweni hodari na wa mioyo ya ushujaa; kwa kuwa ndivyo BWANA atakavyowafanyia adui zenu wote ambao mwapigana nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua akawaambia: “Musiogope, wala musikuwe na wasiwasi, mukuwe imara na hodari, maana hivi ndivyo Yawe atakavyowatendea waadui zenu ambao mutapigana nao. Kwa hiyo, mukuwe imara na hodari.”