Joshua 10:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati jua lilipokuwa karibu kutua, Yoshua aliamuru waondolewe juu ya miti walipokuwa wameangikwa na kutupwa pangoni walimokuwa wamejificha. Kisha wakaweka mawe makubwa kwenye mlango wa pango, nayo mawe hayo yako huko mpaka leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa kuzama jua Yoshua akaamuru, nao wakawashusha kutoka ile miti na kuwatupa kwenye lile pango ambalo walikuwa wamejificha. Wakaweka mawe makubwa kwenye mlango wa pango, ambayo yapo hadi leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakati wa kuchwa jua, Yoshua akatoa amri, nao wakawatelemsha katika hiyo miti, na kuwatupa katika lile pango ambamo walikuwa walijificha kisha wakatia mawe makubwa mdomoni mwa pango, hata hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati jua lilipokuwa karibu kutua, Yoshua aliamuru waondolewe juu ya miti walipokuwa wameangikwa na kutupwa pangoni walimokuwa wamejificha. Kisha wakaweka mawe makubwa kwenye mlango wa pango, nayo mawe hayo yako huko mpaka leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa kuzama jua Yoshua akaamuru wawashushe kutoka kwenye ile miti na kuwatupa kwenye lile pango ambalo walikuwa wamejificha. Kwenye mdomo wa lile pango wakaweka mawe makubwa, ambayo yapo hadi leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa kuzama jua Yoshua akaamuru, nao wakawashusha kutoka kwenye ile miti na kuwatupa kwenye lile pango ambalo walikuwa wamejificha. Kwenye mdomo wa lile pango wakaweka mawe makubwa, ambayo yapo hadi leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakati wa kuchwa jua, Yoshua akatoa amri, nao wakawateremsha katika hiyo miti, na kuwatupa katika lile pango ambamo walikuwa walijificha kisha wakatia mawe makubwa mdomoni mwa pango, hata hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati jua lilipokuwa karibu kutua, Yoshua aliamuru waondolewe juu ya miti walipokuwa wameangikwa na kutupwa pangoni walimokuwa wamejificha. Kisha wakaweka mawe makubwa kwenye mlango wa pango, nayo mawe hayo yako huko mpaka leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa hapo, jua lilipokuchwa, Yosua akatoa amri, ndipo, walipowashusha katika hiyo miti, wakawatupa mle pangoni, walimokuwa walijificha, wakaweka mawe makubwa hapo pa kuliingilia lile pango, nayo yako palepale hata siku hii ya leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakati wa kuchwa jua, Yoshua akatoa amri, nao wakawatelemsha katika hiyo miti, na kuwatupa katika lile pango ambamo walikuwa walijificha kisha wakatia mawe makubwa mdomoni mwa pango, hata hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati jua lilipokuwa karibu kutua, Yoshua aliamuru waondolewe juu ya miti walipokuwa wametundikwa na kutupwa katika pango walimokuwa wamejificha. Kisha wakaweka mawe makubwa kwenye mulango wa pango, nayo mawe hayo yako kule mpaka leo.