Joshua 10:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mwenyezi-Mungu akautia mji huo mikononi mwa Waisraeli, wakauteka mnamo siku ya pili. Waliwaua wakazi wote wa mji huo kama walivyofanya kule Libna.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akautia Lakishi mikononi mwa Israeli, hivyo Yoshua akauteka siku ya pili. Yoshua akauangamiza mji na kila kilichokuwa ndani yake kwa upanga, kama tu vile alivyokuwa ameufanyia mji wa Libna.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akautia huo mji wa Lakishi mkononi mwa Israeli, naye akautwaa siku ya pili, akaupiga kwa makali ya upanga, na wote pia waliokuwamo ndani yake, sawasawa na hayo yote aliyoutenda Libna.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mwenyezi-Mungu akautia mji huo mikononi mwa Waisraeli, wakauteka mnamo siku ya pili. Waliwaua wakazi wote wa mji huo kama walivyofanya kule Libna.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akautia Lakishi mikononi mwa Israeli, Yoshua akauteka siku ya pili. Yoshua akauangamiza mji na kila kilicho ndani yake kwa upanga, kama vile alivyokuwa ameufanyia mji wa Libna.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akautia Lakishi mikononi mwa Israeli, Yoshua akauteka siku ya pili. Yoshua akauangamiza mji na kila kilichokuwa ndani yake kwa upanga, kama tu vile alivyokuwa ameufanyia mji wa Libna.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akautia huo mji wa Lakishi mkononi mwa Israeli, naye akautwaa siku ya pili, akaupiga kwa makali ya upanga, na wote pia waliokuwamo ndani yake, sawasawa na hayo yote aliyoutenda Libna.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mwenyezi-Mungu akautia mji huo mikononi mwa Waisraeli, wakauteka mnamo siku ya pili. Waliwaua wakazi wote wa mji huo kama walivyofanya kule Libna.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akautia Lakisi mikononi mwa Waisiraeli, wakauteka siku ya pili, wakawapiga kwa ukali wa panga wote pia waliokuwamo, wakawafanyizia yote, waliyowafanyizia Walibuna.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akautia huo mji wa Lakishi mkononi mwa Israeli, naye akautwaa siku ya pili, akaupiga kwa makali ya upanga, na wote pia waliokuwamo ndani yake, sawasawa na hayo yote aliyoutenda Libna.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yawe akautia muji huo katika mikono ya Waisraeli, wakauteka kisha siku mbili. Waliwaua wakaaji wote wa muji huo kama walivyofanya kule Libuna.