Joshua 10:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, mfalme Horamu wa Gerezi akaamua kuja kuwasaidia watu wa Lakishi. Lakini Yoshua alimuua pamoja na watu wake wote, hakumbakiza hata mtu mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo huo, Horamu mfalme wa Gezeri alikuwa amepanda ili kusaidia Lakishi, lakini Yoshua akamshinda pamoja na jeshi lake, hadi hapakubakia mtu yeyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati huo Horamu, mfalme wa Gezeri, akakwea ili kuusaidia Lakishi, lakini Yoshua akampiga yeye na watu wake, hata asimsazie hata mtu mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, mfalme Horamu wa Gerezi akaamua kuja kuwasaidia watu wa Lakishi. Lakini Yoshua alimuua pamoja na watu wake wote, hakumbakiza hata mtu mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo huo, Horamu mfalme wa Gezeri alikuwa amepanda ili kusaidia Lakishi, lakini Yoshua akamshinda yeye pamoja na jeshi lake, hadi alipowaangamiza wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo huo, Horamu mfalme wa Gezeri alikuwa amepanda ili kusaidia Lakishi, lakini Yoshua akamshinda pamoja na jeshi lake, hadi hapakubakia mtu yeyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati huo Horamu, mfalme wa Gezeri, akakwea ili kuusaidia Lakishi, lakini Yoshua akampiga yeye na watu wake, hata asimsazie hata mtu mmoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, mfalme Horamu wa Gerezi akaamua kuja kuwasaidia watu wa Lakishi. Lakini Yoshua alimuua pamoja na watu wake wote, hakumbakiza hata mtu mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizo ndipo, Horamu, mfalme wa Gezeri, alipopanda kuusaidia mji wa Lakisi, lakini Yosua akampiga pamoja na watu wake, asisaze kwake hata mmoja aliyekimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati huo Horamu, mfalme wa Gezeri, akakwea ili kuusaidia Lakishi, lakini Yoshua akampiga yeye na watu wake, hata asimsazie hata mtu mmoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo, mufalme Horamu wa Gerezi akaamua kuja kuwasaidia watu wa Lakisi. Lakini Yoshua akamwua pamoja na watu wake wote, hakuacha hata mutu mumoja.