Joshua 10:40 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yoshua aliiteka nchi yote; aliwashinda wafalme wa sehemu za milimani, eneo la Negebu, na sehemu za nchi tambarare na miteremko. Hakuacha chochote chenye uhai ila aliangamiza kila kitu kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Yoshua akalishinda eneo hilo lote, ikiwa ni pamoja na nchi ya vilima, na Negebu, na Shefela, miteremko ya milima, pamoja na wafalme wake wote. Hakubakiza mtu yeyote. Akaangamiza kabisa kila kitu chenye pumzi, kama vile Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alivyokuwa ameamuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya matelemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa wavuta pumzi, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yoshua aliiteka nchi yote; aliwashinda wafalme wa sehemu za milimani, eneo la Negebu, na sehemu za nchi tambarare na miteremko. Hakuacha chochote chenye uhai ila aliangamiza kila kitu kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yoshua akashinda eneo hilo lote, ikiwa ni pamoja na nchi ya vilima, Negebu, sehemu ya magharibi chini ya vilima, matelemko ya milima, pamoja na wafalme wake wote. Hakubakiza humo mtu ye yote. Akaangamiza kabisa kila kitu chenye pumzi, kama vile BWANA, Mungu wa Israeli, alivyokuwa ameamuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Yoshua akalishinda eneo hilo lote, ikiwa ni pamoja na nchi ya vilima, na Negebu, na sehemu ya magharibi chini ya vilima, materemko ya milima, pamoja na wafalme wake wote. Hakubakiza mtu yeyote. Akaangamiza kabisa kila kitu chenye pumzi, kama vile bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa ameamuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya materemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa hai, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yoshua aliiteka nchi yote; aliwashinda wafalme wa sehemu za milimani, eneo la Negebu, na sehemu za nchi tambarare na miteremko. Hakuacha chochote chenye uhai ila aliangamiza kila kitu kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Yosua alivyoipiga hiyo nchi yote, ile ya milimani nayo ya kusini nayo ya nchi ya tambarare nayo ya matelemko pamoja na wafalme wao, hakusaza hata mmoja aliyekimbia. Wenye kuvuta pumzi wote akawatia mwiko wa kuwapo, wasiachwe kabisa, kama Bwana Mungu wa Isiraeli alivyoagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yoshua akaipiga nchi hiyo yote, nchi ya vilima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela, na nchi ya matelemko, na wafalme wake wote; hakumwacha aliyesalia hata mmoja; lakini akawaharibu kabisa wote waliokuwa wavuta pumzi, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yoshua aliiteka inchi yote; akawashinda wafalme wa sehemu za milima, eneo la Negebu, na sehemu za inchi ya bonde na miteremuko. Hakuacha kitu chochote chenye uzima lakini aliangamiza kila kitu kama vile Yawe, Mungu wa Israeli, alivyoamuru.