Joshua 11:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia aliiteketeza miji ile mingine yote kwa moto na kuwaua wafalme wao wote kama Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, alivyomwamuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake, na akawaua kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, jinsi Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyowaagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena miji yote ya wafalme hao, na wafalme wake wote, Yoshua akawatwaa, akawapiga kwa makali ya upanga, na kuwaangamiza kabisa; vile vile kama huyo Musa mtumishi wa Bwana alivyomwamuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia aliiteketeza miji ile mingine yote kwa moto na kuwaua wafalme wao wote kama Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, alivyomwamuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake na kuwapiga kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, kama Mose mtumishi wa BWANA alivyowaagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake na kuwapiga kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, jinsi Musa mtumishi wa bwana alivyowaagiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena miji yote ya wafalme hao, na wafalme wake wote, Yoshua akawatwaa, akawapiga kwa makali ya upanga, na kuwaangamiza kabisa; vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyomwamuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia aliiteketeza miji ile mingine yote kwa moto na kuwaua wafalme wao wote kama Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, alivyomwamuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo miji yote ya hao wafalme Yosua akaiteka pamoja na wafalme wao, akawapiga kwa ukali wa panga akiwatia mwiko wa kuwapo, wasiachwe kabisa, kama Mose, mtumishi wa Bwana, alivyowaagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena miji yote ya wafalme hao, na wafalme wake wote, Yoshua akawatwaa, akawapiga kwa makali ya upanga, na kuwaangamiza kabisa; vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyomwamuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile aliiteketeza miji ile mingine yote kwa moto na kuwaua wafalme wao wote kama vile Musa, mutumishi wa Yawe, alivyomwamuru.