Joshua 11:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amri hii alipewa Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, naye Mose akamwamuru Yoshua ambaye aliitekeleza. Yoshua alitimiza kila jambo Mwenyezi-Mungu alilomwamuru Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa mtumishi wake, vivyo hivyo Musa alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya vivyo hivyo; hakukosa kufanya lolote katika yale yote Mwenyezi Mungu aliyomwagiza Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vile vile kama Bwana alivyomwamuru Musa mtumishi wake, ndivyo Musa alivyomwamuru Yoshua; naye Yoshua akafanya vivyo; hakukosa kufanya neno lo lote katika hayo yote Bwana aliyomwamuru Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amri hii alipewa Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, naye Mose akamwamuru Yoshua ambaye aliitekeleza. Yoshua alitimiza kila jambo Mwenyezi-Mungu alilomwamuru Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile BWANA alivyomwagiza Mose mtumishi wake, vivyo hivyo Mose alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya kama vile alivyoagizwa, akafanya yote kwa uangalifu kama vile BWANA alivyomwagiza Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile bwana alivyomwagiza Musa mtumishi wake, vivyo hivyo Musa alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya kama vivyo, hakukosa kufanya lolote katika yale yote bwana aliyomwagiza Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa mtumishi wake, ndivyo Musa alivyomwamuru Yoshua; naye Yoshua akafanya hivyo; hakukosa kufanya neno lolote katika hayo yote BWANA aliyomwamuru Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amri hii alipewa Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, naye Mose akamwamuru Yoshua ambaye aliitekeleza. Yoshua alitimiza kila jambo Mwenyezi-Mungu alilomwamuru Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama Bwana alivyomwagiza mtumishi wake Mose, ndivyo, Mose naye alivyomwagiza Yosua, navyo ndivyo, Yosua alivyovifaanya: yale maneno yote, Bwana aliyomwagiza Mose, hakutengua hata moja, asilifanye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa mtumishi wake, ndivyo Musa alivyomwamuru Yoshua; naye Yoshua akafanya vivyo; hakukosa kufanya neno lo lote katika hayo yote BWANA aliyomwamuru Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa mutumishi wa Yawe aliipewa amri hii, naye Musa akamwamuru Yoshua ambaye aliitimiza. Yoshua alitimiza kila jambo Yawe alilomwamuru Musa.