Joshua 11:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilikuwa ni matakwa ya Mwenyezi-Mungu mwenyewe kuishupaza mioyo ya watu wa mataifa hayo ili wapigane. Alikusudia wasihurumiwe ila wateketezwe. Ndivyo Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Mwenyezi Mungu mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, awafutilie mbali pasipo huruma, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa lilikuwa ni la Bwana kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile Bwana alivyomwamuru Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilikuwa ni matakwa ya Mwenyezi-Mungu mwenyewe kuishupaza mioyo ya watu wa mataifa hayo ili wapigane. Alikusudia wasihurumiwe ila wateketezwe. Ndivyo Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ni BWANA mwenyewe ambaye aliifanya mioyo yao iwe migumu ili kupigana vita dhidi ya Israeli ili kwamba apate kuwafutilia mbali, pasipo huruma, kama BWANA alivyomwagiza Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana bwana mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli ili apate kuwafutilia mbali pasipo huruma, kama bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa lilikuwa kusudi la BWANA kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile BWANA alivyomwamuru Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilikuwa ni matakwa ya Mwenyezi-Mungu mwenyewe kuishupaza mioyo ya watu wa mataifa hayo ili wapigane. Alikusudia wasihurumiwe ila wateketezwe. Ndivyo Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hili nalo lilitoka kwa Bwana, akiishupaza mioyo yao, waende kupiga vita na Waisiraeli, ule mwiko wa kuwapo waliotiwa umalizike, wasijipatie upendeleo, ila mwangamizo wao tu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa lilikuwa ni la BWANA kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile BWANA alivyomwamuru Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilikuwa ni mapenzi ya Yawe mwenyewe kuifanya mioyo ya watu wa mataifa hayo kuwa migumu kusudi wapigane. Alikusudia wasihurumiwe lakini wateketezwe. Ndivyo Yawe alivyomwamuru Musa.