Joshua 11:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yoshua akaitwaa nchi yote kulingana na yote yale Mwenyezi-Mungu aliyomwambia Mose. Yoshua akaikabidhi kwa Waisraeli iwe mali yao, wagawane kulingana na makabila yao. Kisha nchi nzima ikatulia, ikawa haina vita tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwagiza Musa, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kulingana na walivyogawanyika katika makabila yao. Ndipo nchi ikawa na amani bila vita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote Bwana aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa kabila zao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yoshua akaitwaa nchi yote kulingana na yote yale Mwenyezi-Mungu aliyomwambia Mose. Yoshua akaikabidhi kwa Waisraeli iwe mali yao, wagawane kulingana na makabila yao. Kisha nchi nzima ikatulia, ikawa haina vita tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kama BWANA alivyokuwa amemwagiza Mose, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kama walivyogawanyika katika kabila zao. Ndipo nchi ikawa na amani bila vita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kama vile bwana alivyokuwa amemwagiza Musa, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kulingana na walivyogawanyika katika kabila zao. Ndipo nchi ikawa na amani bila vita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa makabila yao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yoshua akaitwaa nchi yote kulingana na yote yale Mwenyezi-Mungu aliyomwambia Mose. Yoshua akaikabidhi kwa Waisraeli iwe mali yao, wagawane kulingana na makabila yao. Kisha nchi nzima ikatulia, ikawa haina vita tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yosua akaichukua hiyo nchi yote nzima, kama Bwana alivyomwambia Mose, kisha Yosua akaigawia Waisiraeli, iwe fungu lao, kama walivyogawanyika kwa mashina yao. Kisha nchi ikapata kutulia, kwani vita vilikuwa vimekoma
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa kabila zao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yoshua akaitwaa inchi yote kulingana na yote yale Yawe aliyomwambia Musa. Yoshua akaipatia Waisraeli ikuwe mali yao, wagawanyane kulingana na makabila yao. Kisha inchi nzima ikatulia, ikakuwa haina vita tena.