Joshua 11:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakatoka wote na majeshi yao makubwa. Nao walikuwa wengi kama mchanga wa pwani pamoja na magari mengi na farasi wengi sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaja na vikosi vyao vyote na idadi kubwa ya farasi na magari ya vita: jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakatoka nje, wao na jeshi zao zote pamoja nao, watu wengi mno, kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi, pamoja na farasi na magari mengi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakatoka wote na majeshi yao makubwa. Nao walikuwa wengi kama mchanga wa pwani pamoja na magari mengi na farasi wengi sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaja na vikosi vyao vyote na hesabu kubwa ya magari ya kuvutwa na farasi, jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaja na vikosi vyao vyote na hesabu kubwa ya farasi na magari ya kuvutwa na farasi, jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakatoka nje, wao na majeshi yao yote pamoja nao, watu wengi mno, kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi, pamoja na farasi na magari mengi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakatoka wote na majeshi yao makubwa. Nao walikuwa wengi kama mchanga wa pwani pamoja na magari mengi na farasi wengi sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakatoka wao pamoja na majeshi yao, wakawa watu wengi, kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari ulivyo mwingi; walikuwa hata na farasi na magari mengi sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakatoka nje, wao na jeshi zao zote pamoja nao, watu wengi mno, kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi, pamoja na farasi na magari mengi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wakatoka wote na makundi yao makubwa ya waaskari. Nao walikuwa wengi kama muchanga wa bahari pamoja na magari mengi na farasi wengi sana.