Joshua 12:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafuatao ndio wafalme ambao Waisraeli waliwashinda na kuchukua nchi yao yote iliyokuwa mashariki ya mto Yordani kutoka bonde la mto Arnoni mpaka mlima Hermoni na nchi yote ya Araba upande wa mashariki:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kumiliki maeneo yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni hadi Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki mwa Araba:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafuatao ndio wafalme ambao Waisraeli waliwashinda na kuchukua nchi yao yote iliyokuwa mashariki ya mto Yordani kutoka bonde la mto Arnoni mpaka mlima Hermoni na nchi yote ya Araba upande wa mashariki:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli walikuwa wamewashinda na kutawala nchi yao upande wa mashariki ya Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa mawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafuatao ndio wafalme ambao Waisraeli waliwashinda na kuchukua nchi yao yote iliyokuwa mashariki ya mto Yordani kutoka bonde la mto Arnoni mpaka mlima Hermoni na nchi yote ya Araba upande wa mashariki:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa ndio wafalme wa nchi hii, wana wa Israeli waliowapiga, walipoichukua nchi yao, iwe yao wenyewe ng'ambo ya huko ya Yordani upande wa maawioni kwa jua toka mto wa Arnoni mpaka milimani kwa Hermoni, nayo nyika hiyo yote iliyoko upande wa maawioni kwa jua:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng’ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawa ndio wafalme ambao Waisraeli waliwashinda na kunyanganya inchi yao yote iliyokuwa upande wa mashariki wa muto Yordani kutokea bonde la muto Arnoni mpaka kwenye mulima Hermoni na inchi yote ya Araba upande wa mashariki: