Joshua 12:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Sihoni wa Waamori aliyeishi huko Heshboni na kutawala kutoka makao yake makuu huko Aroeri, mji uliokuwa kandokando ya bonde la Arnoni. Alitawala pia kuanzia katikati ya bonde hadi mto Yaboki ambao ulikuwa mpaka wa nchi ya Waamoni, yaani nusu ya nchi ya Gileadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hata kuufikilia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Sihoni wa Waamori aliyeishi huko Heshboni na kutawala kutoka makao yake makuu huko Aroeri, mji uliokuwa kandokando ya bonde la Arnoni. Alitawala pia kuanzia katikati ya bonde hadi mto Yaboki ambao ulikuwa mpaka wa nchi ya Waamoni, yaani nusu ya nchi ya Gileadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ni pamoja na nusu ya Gileadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hadi kuufikia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Sihoni wa Waamori aliyeishi huko Heshboni na kutawala kutoka makao yake makuu huko Aroeri, mji uliokuwa kandokando ya bonde la Arnoni. Alitawala pia kuanzia katikati ya bonde hadi mto Yaboki ambao ulikuwa mpaka wa nchi ya Waamoni, yaani nusu ya nchi ya Gileadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni na kutawala toka Aroeri ulioko kwenye mto wa Arnoni kuanzia mle mtoni katikati kufikia nusu ya Gileadi mpaka mto wa Yaboko, mpaka wa wana wa Amoni uliko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hata kuufikilia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Sihoni wa Waamori aliyeishi kule Hesiboni na kutawala kutokea kwenye makao yake makubwa kule Aroeri, muji uliokuwa kandokando ya bonde la Arnoni. Alitawala vilevile kuanzia katikati ya bonde mpaka kwenye muto Yaboki ambao ulikuwa mupaka wa inchi ya Waamoni, ni kusema nusu ya inchi ya Gileadi.