Joshua 12:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vilevile, alitawala nchi yote ya Araba, kutoka bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki, mpaka Beth-yeshimothi kwenye Bahari ya Chumvi na kuendelea mpaka chini ya mlima Pisga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya miteremko ya Pisga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Ataba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya matelemko ya Pisga;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vilevile, alitawala nchi yote ya Araba, kutoka bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki, mpaka Beth-yeshimothi kwenye Bahari ya Chumvi na kuendelea mpaka chini ya mlima Pisga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya matelemko ya Pisga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Araba, mpaka Bahari ya Chumvi, kuelekea mashariki, njia ya kwenda Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya materemko ya Pisga;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vilevile, alitawala nchi yote ya Araba, kutoka bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki, mpaka Beth-yeshimothi kwenye Bahari ya Chumvi na kuendelea mpaka chini ya mlima Pisga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliitawala nayo nyika kufikia upande wa maawioni kwa jua wa bahari ya Kineroti mpaka upande wa maawioni kwa jua wa bahari ya nyikani, ndiyo Bahari ya Chumvi, ukifuata njia ya kwenda Beti-Yesimoti, tena kusini chini ya matelemko ya Pisiga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Ataba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya matelemko ya Pisga;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, alitawala inchi yote ya Araba, kutokea bahari ya Kineroti, upande wa mashariki, mpaka Beti-Yesimoti kwenye bahari ya Chumvi na kuendelea mpaka chini ya mulima Pisiga.